Huduma Ya Kuunganishiwa Majisafi
Imewekwa: 06 October, 2024

Ili uweze kupata huduma ya maunganisho mapya ya maji tafadhali zingatia yafuatayo:
- Unatakiwa kufika ofisi za Tanga UWASA zilizo karibu nawe kwa ajili ya kufungua faili la maombi ya kuunganishwa na huduma ya maji safi (kwa ajili ya kuwekea taarifa muhimu).
- Utachukuliwa maelezo na Afisa anayehusika na masuala ya maunganisho mapya ikiwemo majina matatu, eneo, (kitalu na block number) kwa wale waliopo kwenye maeneo yaliyopimwa
- Utatakiwa kuleta nakala ya kielelezo cha umiliki(hati, ofa…) pamoja na barua ya Mwenyekiti wa Mtaa
- Utapewa fundi atakaye kwenda ndani ya siku saba (7) za kazi kukagua eneo litakalo unganishiwa majisafi ili kujua kama eneo hilo lina bomba lililokaribu kutoa huduma.
- Kwa maeneo yenye umbali uliochini ya mita sitini (60), mteja atatakiwa kuwasilisha site plan (kwa eneo lililopimwa)
- Kwa maeneo ambayo bomba kubwa la kusambaza maji lipo mbali zaidi ya mita sitini (60) mteja atashauriwa kusubiri Tanga UWASA isogeze huduma eneo hilo ili kuwafikia wateja wengi zaidi.
- Kwa umbali unaozidi mita 60 fundi aliyefanya ukaguzi atawasiliana na Msimamizi wake kabla ya kumruhusu mteja kuwasilisha taarifa zake (angalia na.4)
- Orodha ya vifaa vingine pamoja na mita, gharama za kuchimba mtaro na kufukia zitaandaliwa na mteja atapewa namba ya malipo ya serikali (GePG) akalipie.
- Baada ya kulipa kikamilifu gharama zote, fundi atakabidhiwa vifaa tayari kwa kuunganisha huduma ya majisafi ndani ya siku saba (7) za kazi.
TAHADHARI: EPUKA VISHOKA FIKA OFISINI KUPATA HUDUMA HII
HAKUNA MALIPO YA AWALI, MALIPO HUFANYIKA KWA MKUPUO MOJA BAADA YA FUNDI KUANDAA ORODHA YA VIFAA NA GHARAMA
MALIPO YOTE HUFANYIKA KUPITIA MFUMO WA MALIPO YA SERIKALI (GePG) KUPITIA NAMBA YA MALIPO YA SERIKALI ITAKAYOTOLEWA OFISINI