TAARIFA YA KUHAMA KWA OFISI ZA HUDUMA KWA WATEJA PANGANI
Imewekwa: 09 March, 2026
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) anawataarifu wateja a wananchi wote wa eneo la kihuduma la Pangani Mjini kuwa Ofisi za Huduma kwa Wateja kanda ya Pangani zimehamia katika eneo la MKOMA karibu na ofisi za RUWASA njia ya kwenda Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani kuanzia tarehe 09.03.2026.
Hivyo tunawakaribisha wateja na wananchi wote kuendelea kupata huduma zetu.

