Kuunganishwa na Majitaka
Imewekwa: 06 October, 2024

JINSI YA KUJIUNGA NA MFUMO WA MAJITAKA
IKUMBUKWE: KIGEZO CHA KUZINGATIWA KWA MTEJA KUUNGANISHWA NA MFUMO WA MAJITAKA SHARTI AWE NA MFUMO WA MAJISAFI (AWE AMEUNGANISHWA NA HUDUMA YA MAJISAFI).
- Mteja wa maji safi aliyeko karibu na mfumo wa maji taka anaweza kuunganishwa.
- Mwombaji atafika ofisi za mamlaka na atatupatia taarifa zake jina kamili, anuani ya eneo, namba ya simu na akaunti yake ya maji.
- Fundi atatembelea eneo lake kwa upimaji kuangalia uwezekano wa kuungwa kwenye mtandao wa maji taka na atajaza taarifa zote katika fomu maalum ya maombi.
- Mwombaji atatarifiwa juu ya matokeo ya upimaji na gharama husika zitakazohusisha gharama ya maunganisho, gharama ya vifaa na ufundi.
- Mwombaji atafika ofisi za mamlaka kupata hati ya madai na namba ya kumbukumbu ya kufanya malipo ili aweze kulipia katika mfumo wa serikali.
- Baada ya kuthibitisha malipo fundi atafanya kazi ndani ya siku za kazi zisizopungua saba