Ninatoaje taarifa juu ya uvujaji wa maji?
Imewekwa: 27 December, 2024
Kuna namna nyingi ya kuweza kutufikia ili kutoa taarifa za uvujaji na masuala mengine kama ifuatavyo:
- Unaweza kutoa taarifa juu ya kuvuja maji, kuziba kwa mtandao wa majitaka, na wizi wa maji kwa kupiga namba za bure 0800110111
- Unaweza kutoa taarifa kwa kufika ofisi za Tanga UWASA zilizo karibu nawe.
- Unaweza kutoa taarifa kwa mtumishi yeyote wa Tanga UWASA kuhusu suala au tatizo lolote linalokutatiza