Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TANGA

(Tanga UWASA)

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
/

Vyanzo vya Maji na Uhifadhi wa Mazingira

Imewekwa: 18 August, 2026
Vyanzo vya Maji na Uhifadhi wa Mazingira

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) ina vyanzo vipatavyo 20 vya maji vinavyohusisha Mto Zigi unaopatikana katika Milima ya Amani Wilayani Muheza, Chanzo cha maji cha Magoroto Wilayani Muheza, Kisima 1 kilichopo Mwakileo Jijini Tanga, Visima 4 vilivyopo Boza wilayani Pangani na Visima 12 Muheza vinavyotumika kwa ajili ya kusambaza maji katika maeneo mbalimbali ya kihuduma.

Katika kuendelea kuhakikisha upaikanaji wa maji ya uhakika Mamlaka inajihusisha pia na shughuli za uhifadhi wa mazingira katika vyanzo vya maji kupitia utekelezaji wa programs maalum ikiwemo upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali na kushirikiana na jamii zinazozunguka vynazo vya maji, ambapo kwa sasa Tanga UWASA inafanya kazi kwa ukaribu na Umoja wa Wakulima Wahifadhi Mazingira Kihuwhi Zigi (UWAMAKIZI) wanaopatikana wilayani Muheza, ambapo taasisi inashiriki kufanikisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi mazingira zinazolenga kuendelea kutunza vyanzo vya maji na kufanikisha upatikanaji wa maji ya uhakika.