Huduma ya Majitaka
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) inajihusisha na utoaji wa huduma ya uondoshaji majitaka katika makazi na majengo ya wananchi katika maeneo ya kihuduma ya Tanga Jiji pamoja na Miji ya Muheza na Pangani kwa kutumia njia mbili ambazo zinahusisha Mtandao wa mabomba yaliyopita na kuunganishwa moja kwa moja katika majengo ya wananchi ambao una urefu wa Kilomita 42.14 na kwa sasa mtandao umepita katika maeneo ya Kata za USAGARA, NGAMIANI KATI, KUSINI, KASKAZINI, RASKAZONE, CHUMBAGENI NA CENTRAL na jumla ya wateja 3,164 wameunganishwa na huduma hiyo kwa Tanga Jiji.
Tanga UWASA pia inatoa huduma ya uondoshaji Majitaka kwa kutumia Magari Maalum kwa wateja wote ambao hawajafikiwa na mtandao wa majitaka na gharama za huduma hutegemeana na umbali wa wateja ambapo 0- 5km gharama ni 50,000, 6-10km gharama ni 80,000 na 11-15 km gharama ni 100,000 na umbali ukiwa zaidi ya hapo mteja ataongeza 2000 kila kilometa

