Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TANGA

(Tanga UWASA)

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
/ News

Wakala wa Vipimo wahakiki ufanisi wa Mita za maji za Tanga UWASA

Imewekwa: 28 September, 2026
Wakala wa Vipimo wahakiki ufanisi wa Mita za maji za Tanga UWASA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA), kwa kushirikiana na Wakala wa Vipimo nchini (WMA), imefanya zoezi maalumu la uhakiki wa mita za maji zenye umri wa zaidi ya miaka miwili katika Mtaa wa Raskazone, Kata ya Central, Jijini Tanga.

Zoezi hilo linalenga kuhakiki usahihi na ufanisi wa mita zinazotumiwa na wateja, ili kuhakikisha vipimo vinavyotumika katika matumizi na malipo ya huduma ya maji vinafanyika kwa usahihi. Aidha kupitia zoezi hilo Wakala wa vipimo wanalenga kuhakiki mita za wateja 150 wa Tanga UWASA kila mwisho wa mwezi, katika maeneo mbalimbali ya kihuduma

Tanga UWASA inawasihi wateja wake kutoa ushirikiano kwa watumishi wanaotekeleza zoezi hilo katika maeneo mbalimbali.