Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TANGA

(Tanga UWASA)

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
/ News

MWENGE WA UHURU WARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI MRADI WA MAJI - MZIZIMA

Imewekwa: 23 June, 2026
MWENGE WA UHURU WARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI MRADI WA MAJI - MZIZIMA

Mwenge wa Uhuru 2026 umetembelea na kukagua mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya kuboresha upatikanaji wa majisafi Mzizima - Mikocheni katika kata ya Mzizima, Mradi unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) na kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumza baada ya kukagua Mradi huo na kushiriki katika zoezi la kumuunganishia mteja mpya huduma ya majisafi, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru  Kitaifa Ndugu. Wazo Michael Mwang'onda amesema dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Awamu ya sita ni kuendelea mkakati wa kumtua mama ndooo kichwani na hii inajidhihilisha wazi kupitia miradi mbalimbali ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa na sekta ya maji nchini na ameipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) Kwa utekelezaji mzuri wa mradi na kuendelea kusogeza huduma karibu na wananchi.

Kwa upande wake Msimamizi wa mradi huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 233.4, Mhandisi Aaron Chanimbaga akisoma taarifa ya mradi ameainisha kuwa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 50 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mapema ifikapo mwezi Septemba 2026 na utawanufaisha zaidi ya wananchi 4,780 kwa kuboresha upatikanaji wa huduma ya uhakika.

Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2026 zinaongozwa na Kauli Mbiu isemayo “Tanzania ni yetu sote tushirikiane kwa pamoja kuleta maendeleo”