Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TANGA

(Tanga UWASA)

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
/ News

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MAJI NA MAZINGIRA YARIDHISHWA NA KAZI YA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI TANGA

Imewekwa: 17 March, 2026
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MAJI NA MAZINGIRA YARIDHISHWA NA KAZI YA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI TANGA

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeendelea na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali chini ya wizara ya Maji katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo leo tarehe 17.03.2026 Wajumbe wa kamati wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati Mhe. Jackson Kiswaga wametembelea na kujionea maendeleo ya utekelezaji mradi wa Kuboresha hali ya upatikanaji maji Tanga awamu ya tatu kupitia ufadhili wa Hatifungani ya Kijani (Tanga Water Green Bond) unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) lengo kuu ikiwa ni kuimarisha hali ya upatikanaji wa huduma ya uhakika kwa wakazi wa Mradi huu wa Jiji la Tanga, pamoja na Miji ya Muheza na Pangani.

Aidha Kamati ilifika pia kukagua maendeleo ya utekelezaji ya mradi wa maji wa Mkinga-Horohoro ambao utakwenda kuhudumia vijiji 37 vya wilaya ya Mkinga na kuondoa ambao umefikia asilimia 65 ya utekelezaji wake sambamba na kushuhudia kukamilika kwa hatua ya kwanza ya kufanikisha upatikanaji wa maji katika kijiji cha Mtimbwani ambapo maji yanatoka bombani.

Wajumbe wa kamati wakiongozwa na na Mwenyekiti wa kamati Mhe. Jackson Kiswaga wameipongeza Serikali na watendaji wa Wizara ya maji Mkoani Tanga kwa kazi nzuri inayofanyika katika kusimamia utekelezaji wa miradi na kupongeza utaratibu shirikishi wa mfumo wa Hatifungani ya Kijani (Tanga Water Green Bond) katika kutekeleza miradi mikubwa ya maji.

Awali Wajumbe wa Kamati wakiongozana na Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso (Mb)walipata taarifa ya hali ya upatikanaji wa Maji katika Mkoa wa Tanga kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Balozi. Dkt. Batilda Burian