Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TANGA

(Tanga UWASA)

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
/ News

HATIFUNGANI YA TANGA UWASA, MAGEUZI KATIKA SEKTA YA MAJI NCHINI

Imewekwa: 21 July, 2026
HATIFUNGANI YA TANGA UWASA, MAGEUZI KATIKA SEKTA YA MAJI NCHINI

HATIFUNGANI YA TANGA UWASA, MAGEUZI KATIKA SEKTA YA MAJI NCHINI

Mradi wa Hatifungani ya Kijani wa Tanga UWASA umeendelea kupongezwa kwa mafanikio yake katika kuboresha upatikanji wa huduma ya maji kwa jamii,  hayo yameanishwa wakati wa Ziara ya Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mkoani Tanga.

Mwenyeji wa ziara hiyo, Waziri wa Maji wa Tanzania Bara Mhe. Juma Aweso (Mb), amesema mafanikio hayo yameifanya Wizara ya Maji kuanzisha mfumo mbadala wa upatikanaji wa fedha (Alternative Financing) kwa kushirikisha jamii na sekta binafsi ili kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maji nchini, ambapo tayari Mamlaka zote za maji nchini zimeelekezwa kujipanga kutumia mfumo huo kutokana na matokeo chanya yaliyopatikana Tanga.

Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Nadir Abdul-Latif Alwardy, ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Maji na Tanga UWASA kwa ubunifu huo, akisema umefungua ukurasa mpya wa uwekezaji katika sekta ya maji na kuwa Zanzibar itatumia uzoefu huo kuboresha huduma za maji visiwani.

Kupitia Hatifungani ya Kijani, Tanga UWASA imekusanya Shilingi bilioni 53.12, zitakazoongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 45 hadi milioni 60 kwa siku na kuboresha upatikanaji wahuduma ya uhakika kwa wananchi.