Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TANGA

(Tanga UWASA)

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
/ News

TANGA UWASA YATETA NA WADAU, MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI

Imewekwa: 19 March, 2026
TANGA UWASA YATETA NA WADAU, MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI

Katika muendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Maji kwa mwaka 2026, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) kupitia vitengo vya Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa wateja imeendelea kutoa elimu kwa umma juu ya huduma zinazotolewa na taasisi, ambapo leo tarehe 19 Machi, taasisi imetoa elimu kupitia Radio Nuur ambapo pamoja na mada nyingine taasisi pia ilitoa mada juu ya Matumizi ya mfumo mpya wa maombi ya huduma kwa njia ya mtandao (MajiOAP) na Utambulisho wa Kanda za kihuduma za Tanga UWASA.

Sambamba na utoaji wa elimu wataalamu pia walitumia fursa hiyo kuwakukmbusha wateja waliositishiwa huduma kuwa Ofa ya kurejeshewa huduma bila tozo bado inaendelea hadi tarehe 31 Machi, 2026 hivyo wafike katika ofisi za Tanga UWASA zilizopo karibu nao kupata utaratibu wa kurejeshewa huduma na makubaliano ya kufanya malipo ya madeni yao.

Maadhimisho ya Wiki ya Maji kwa mwaka 2026 yanabebwa na kauli mbiu isemayo "Rasilimali za maji na Usawa wa Kijinsia".