SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2026
Imewekwa: 06 March, 2026
Watumishi wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) ni miongoni mwa washiriki katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ngazi ya Wilaya, ambapo kwa wilaya ya Tanga maadhimisho hayo yalifanyika katika viwanja vya Usagara na kilele chake ni tarehe 08.03.2026 Wilayani Korogwe.
Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanabebwa na kauli mbiu isemayo; "Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana msingi jumuishi wa maendeleo kufikia Dira 2050"

