ZOEZI LA UFUNGAJI WA MITA ZA PREPAID ZA MRADI WA HATIFUNGANI LAANZA RASMI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) kupitia mafundi sanifu wa kitengo cha huduma kwa wateja imeanza rasmi zoezi la ufungaji wa mita za kisasa za malipo kabla (Pre - paid Water Meters) kama sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Hatifungani ambapo kupitia mradi huo jumla ya mita 10,000 zinatarajiwa kufungwa kwa wateja katika maeneo ya kihuduma ya Jiji la Tanga pamoja na Miji ya Muheza na Pangani.
Katika zoezi hilo zaidi ya mita 40 zimefungwa kwa wateja katika taasisi za Umma pamoja na wateja wenye madeni makubwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Tanga na linaendelea katika maeneo mengine.
Utekelezaji wa zoezi hilo ni muendelezo wa utimizaji wa lengo la kuanza rasmi kwa matumizi ya dira za malipo ya kabla katika sekta ya Maji Nchini na jitihada za taasisi za kuendelea kuimarisha makusanyo na kuchochea matumizi sahihi ya maji.

