Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TANGA

(Tanga UWASA)

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
/ News

UFADHILI WA UMMA NA UWEKEZAJI ENDELEVU KATIKA SEKTA YA MAJI

Imewekwa: 21 August, 2026
UFADHILI WA UMMA NA UWEKEZAJI ENDELEVU KATIKA SEKTA YA MAJI

Uzoefu wa Tanzania katika matumizi ya Hatifungani ya Kijani unaonyesha kile kinachowezekana pale ambapo mageuzi katika sekta ya maji yanaambatana na mbinu bunifu za ufadhili.

Katika Kongamano la Viongozi wa Sekta za Maji na Usafi wa Mazingira Africa lilofanyika Kigali nchini Rwanda, Bw. Alawi Ahmadi, akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) ameainisha uzoefu wa Tanzania wa kuvuka utegemezi wa ufadhili wa kawaida wa ndani na kuelekea katika kuvutia mitaji binafsi kupitia mfumo wa Hatifungani ya Kijani.

Kongamano hilo limewakutanisha Viongozi na Wataalamu kutoka Afrika kujadili swali muhimu, Tunawezaje kubadilisha miradi ya WASH kutoka kuwa mawazo mazuri hadi kuwa fursa zinazoweza kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi, taasisi na wafadhili wa maendeleo?

Uzoefu wa Tanga UWASA unaonyesha umuhimu wa mbinu hii ya Hatifungani ya kijani kupitia;
• Kupunguza utegemezi wa ufadhili wa kawaida wa Serikali na kuongeza vyanzo bunifu vya fedha.
• Kuimarisha taasisi na mageuzi ya sekta ili kuongeza imani ya wawekezaji.
• Kutumia Hatifungani na mifumo mingine ya kupunguza vihatarishi vya uwekezaji.
• Kuunganisha ufadhili na msaada wa kitaalamu pamoja na kujenga uwezo wa taasisi.
• Kuimarisha uhusiano kati ya mageuzi ya kitaifa, utendaji wa Mamlaka za maji na uwekezaji endelevu.

Ujumbe mkuu katika kongamano hilo ni, "ufadhili wa sekta ya maji si suala la kutafuta fedha zaidi pekee ni suala la kuifanya sekta iwe tayari kwa uwekezaji."

Kupitia mageuzi sahihi, ushirikiano na mifumo bunifu ya ufadhili, maji yanaweza kutoka katika mtazamo wa kuwa gharama ya Serikali pekee na kuwa fursa ya uwekezaji kwa maendeleo, huku tukizingatia uwezo wa wananchi kumudu huduma, uendelevu na thamani ya huduma kwa umma.

Tunajivunia kuona Tanzania ikichangia katika mjadala huu muhimu wa Afrika na kuonyesha kuwa ufadhili na bunifu katika miradi ya sekta ya Maji unawezekana.
#AfricaWaterLeadership #WASH #WaterFinancing #GreenBonds #InnovativeFinance #WaterSecurity #Tanzania #TANGAUWASA #WaterForPeople #D30 #Kigali