Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TANGA

(Tanga UWASA)

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
/ News

WATEJA WAPYA 2,400 KUNUFAIKA KUPITIA MRADI WA HATIFUNGANI YA KIJANI

Imewekwa: 16 July, 2026
WATEJA WAPYA 2,400 KUNUFAIKA KUPITIA MRADI WA HATIFUNGANI YA KIJANI

Jumla ya wateja wapya 2,400 kunufaika na huduma ya majisafi baada ya kukamilika kwa mradi wa Kuboresha hali ya upatikanaji huduma ya maji Tanga awamu ya tatu kupitia ufadhili wa Hatifungani ya Kijani, hayo yamesemwa na Eng. Salum Ngumbi Meneja Mradi kutoka Mamalaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) wakati akitoa taarifa kwa wadau ambao ni viongozi wa Shirika la uwekezaji la ALCB kanda ya Kenya kama sehemu wa wawekezaji wakubwa katika Hatifungani ya Kijani ya Tanga UWASA wakiwa wameambatana na viongozi kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) waliofika Tanga UWASA kwa lengo la kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa Hatifungani unaotarajiwa kukamilika mapema mwaka huu.

Akiwasilisha taarifa ya mradi ambao umefikia asilimia 70,  Eng. Salum Ngumbi, ameainisha kuwa sehemu moja wapo (Project Scope) ya utekelezaji wa mradi ni kusogeza huduma karibu na wateja kupitia uendelezaji wa mtandao wa mabomba na kuunganisha wateja wapya na huduma ya majisafi katika maeneo yao ambapo mpaka sasa jumla ya wateja 1,574 katika Jiji la Tanga na Miji ya Muheza na Pangani wamekwisha unganishiwa na huduma hiyo huku lengo kuu ikiwa ni kufikia wateja 2,400.

Nae kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga UWASA, Eng. Geofrey Hilly, amewashukuru wawekezaji hao  kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha adhma ya Serikali kupitia Wizara ya Maji ya kuendelea kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi kupitia bunifu na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati.