BILIONI 2.1 KUIMARISHA HUDUMA YA MAJITAKA TANGA JIJI
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA), kupitia mradi wa Hatifungani ya Kijani, inaendelea na utekelezaji wa kazi ya ujenzi na ukarabati wa mtandao wa majitaka kwa urefu wa kilomita 3 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Tanga, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha upaikanaji wa huduma ya majitaka na kuimarisha usafi wa mazingira.
Mradi huo unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 2.1 hadi kukamilika kwake na unalenga kuongeza uwezo na ufanisi wa mtandao wa majitaka ili kupanua wigo wa huduma ya majitaka na kuwawezesha wakazi wengi zaidi wa Jiji la Tanga kunufaika na huduma yenye ufanisi.
Mradi huo ni sehemu ya juhudi za Tanga UWASA katika kuhakikisha huduma ya majitaka inakwenda sambamba na ukuaji wa Jiji la Tanga.

