Je wajua njia mbalimbali za kutoa maoni na malalamiko kama mteja?
Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) inapokea na kushughulikia malalamiko kuhusu utoaji wa huduma. Mteja anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa kutumia njia zifuatazo:-
i. Kufika Ofisi za Huduma kwa Wateja (Tanga UWASA).
ii. Kuandika barua pepe (e-mail info@tangauwasa. go.tz) au barua kwa
Mkurugenzi Mtendaji)
iii. Kupiga simu ya bure yenye nambari 0800110111
iv. Kuweka kwenye makundi mbalimbali ya WhatsApp yaliyoanzishwa na ofisi za Tanga UWASA maeneo tofauti tofauti yakiwaunganisha Wateja wanaoishi katika eneo husika. Maoni, malalamiko na mapendekezo yatafuatiliwa na kufanyiwa kazi kwa haraka na kwa mujibu wa viwango vyetu vya huduma. Tanga UWASA inakaribisha mawazo na maoni kutoka kwa wadau ili kuboresha utoaji wa huduma.