Najiunga vipi na mfumo wa mabomba wa majitaka?
Imewekwa: 29 September, 2024
INSI YA KUJIUNGA NA MFUMO WA MAJITAKA
IKUMBUKWE: KIGEZO CHA KUZINGATIWA KWA MTEJA KUUNGANISHWA NA MFUMO WA MAJITAKA SHARTI AWE NA MFUMO WA MAJISAFI (AWE AMEUNGANISHWA NA HUDUMA YA MAJISAFI).
Mteja wa maji safi aliyeko karibu na mfumo wa maji taka anaweza kuunganishwa.
- Mwombaji atafika ofisi za mamlaka na atatupatia taarifa zake jina kamili, anuani ya eneo, namba ya simu na akaunti yake ya maji.
- Fundi atatembelea eneo lake kwa upimaji kuangalia uwezekano wa kuungwa kwenye mtandao wa maji taka na atajaza taarifa zote katika fomu maalum ya maombi.
- Mwombaji ataarifiwa juu ya matokeo ya upimaji na gharama husika zitakazohusisha gharama ya maunganisho, gharama ya vifaa na ufundi.
- Mwombaji atafika ofisi za mamlaka kupata hati ya madai na namba ya kumbukumbu ya kufanya malipo ili aweze kulipia katika mfumo wa serikali.
- Baada ya kuthibitisha malipo fundi atafanya kazi ndani ya siku za kazi zisizozidi saba