Natumia vipi maji kwa uangalifu?
Imewekwa: 29 September, 2024
Vidokezo vya Utunzaji wa Maji
1. Chunguza uvujaji wa mabomba na kwenye mfumo wa maji chooni.
2. Funga mabomba vizuri na hakikisha hakuna matone ya maji yanayodondoka.
3. Wakati wa kuosha vyombo hakikisha huachii maji yakimwagika ovyo (kinga maji kwenye chombo wakati wa kuosha na kusuuza).
4. Tumia muda mfupi wakati wa kuoga endapo unatumia bomba la juu (shower)
5. Funga bomba la maji wakati wa kupiga mswaki.
6. Tumia ufagio kusafisha sakafu (pavements) kabla ya kutumia maji.