MWIZI WA MAJI ABAINIKA DONGE

Imewekwa: Sep, 5 2023


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (TANGA UWASA) kwa kushirikiana na jeshi la Polisi yafanikiwa kubaini mwizi wa maji katika eneo la Donge (Maarufu kama kwa Mama Sigara) ambae alikuwa amejiunganishia huduma kinyume na utaratibu ambapo baada ya kubainika huduma imesitishwa katika eneo hilo mpaka pale taratibu za kisheria zitakapo kamilika.
Akizungumza katika tukio hilo Mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu Saidi Rajabu amesema kuwa mtuhumiwa ni kijana anaeishi peke yake katika makazi hayo na alipopata tetesi za uwepo wa tabia hiyo alianza mara moja jitihada za kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na mafundi wa TANGA UWASA ili kubaini uhalisia ndipo wakafinikiwa kumkamata.
TANGA UWASA inaendelea kuwasisitiza wananchi kutoa taarifa za uwepo wa matukio ya wizi wa maji ili kuzuia upotevu wa maji ambapo donge nono hutolewa kwa taarifa zote zinazothibitishwa.
Sheria Na.5/2019 ya Huduma za maji na Usafi wa Mazingira inazuia matumizi yasiyosahihi ya miundombinu ya huduma sambamba na wizi wa maji ambapo adhabu yake ni malipo ya fine ya hadi Shilingi Milioni 50 au kutumikia kifungo cha hadi Miaka 5 au vyote kwa pamoja.



MWISHO.