Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Vidokezo vya Utunzaji wa Maji

1. Chunguza uvujaji wa mabomba na kwenye mfumo wa maji chooni.

2. Funga mabomba vizuri na hakikisha hakuna matone ya maji yanayodondoka.

3. Wakati wa kuosha vyombo hakikisha huachii maji yakimwagika ovyo (kinga maji kwenye chombo wakati wa kuosha na kusuuza).

4. Tumia muda mfupi wakati wa kuoga endapo unatumia bomba la juu (shower)

7. Funga bomba la maji wakati wa kupiga mswaki.

8. Tumia ufagio kusafisha sakafu (pavements) kabla ya kutumia maji.

JINSI YA KUJIUNGA NA MFUMO WA MAJITAKA

IKUMBUKWE: KIGEZO CHA KUZINGATIWA KWA MTEJA KUUNGANISHWA NA MFUMO WA MAJITAKA SHARTI AWE NA MFUMO WA MAJISAFI (AWE AMEUNGANISHWA NA HUDUMA YA MAJISAFI).

Mteja wa maji safi aliyeko ndani ya umbali wa mita 30 kwenye mfumo wa maji taka anawajibika kujiunga. Hata hivyo kwa mteja yeyote aliyekaribu na mtandao anaweza kuunganishwa.

 • Mwombaji atafika ofisi za mamlaka na atatupatia taarifa zake jina kamili, anuani ya eneo, namba ya simu na akaunti yake ya maji.
 • Fundi atatembelea eneo lake kwa upimaji kuangalia uwezekano wa kuungwa kwenye mtandao wa maji taka na atajaza taarifa zote katika fomu maalum ya maombi.
 • Mwombaji ataarifiwa juu ya matokeo ya upimaji na gharama husika zitakazohusisha gharama ya maunganisho, gharama ya vifaa na ufundi.
 • Mwombaji atafika ofisi za mamlaka kupata hati ya madai na namba ya kumbukumbu ya kufanya malipo ili aweze kulipia katika mfumo wa serikali.
 • Baada ya kuthibitisha malipo fundi atafanya kazi ndani ya siku za kazi zisizopungua saba

Maunganisho Mapya ya Huduma ya Majisafi

Ili uweze kupata huduma ya maunganisho mapya ya maji tafadhali zingatia yafuatayo:

 1. Unatakiwa kufika ofisi za TANGAUWASA zilizo karibu nawe kwa ajili ya kufungua faili la maombi ya kuunganishwa na huduma ya maji safi (kwa ajili ya kuwekea taarifa muhimu).
 2. Utachukuliwa maelezo na Ofisa anayehusika na masuala ya maunganisho mapya ikiwemo majina matatu, eneo, (kitalu na block number) kwa wale waliopo kwenye maeneo yaliyopimwa
 3. Utapewa fundi atakaye kwenda kukagua eneo litakalo unganishiwa majisafi ili kujua kama eneo hilo lina bomba lililokaribu kutoa huduma.
 4. Kwa maeneo ambayo bomba kubwa la kusambaza maji lipo mbali zaidi ya mita hamsini (50) mteja anashauriwa kuomba tawi kwa jirani yake mwenye maji au kuomba TANGAUWASA isogeze huduma eneo hilo (Line Extension) ili kuwafikia wateja wengi zaidi.
 5. Kwa maeneo yenye umbali uliochini ya mita hamsini (50), mteja atatakiwa kuwasilisha site plan (kwa eneo lililopimwa) picha moja passport size (1)
 6. Kwa umbali unaozidi mita 50 fundi aliyefanya ukaguzi atawasiliana na Msimamizi wake kabla ya kumruhusu mteja kuwasilisha taarifa zake (angalia na.4)
 7. Gharama ya vifaa vingine, gharama za kuchimba mtaro na kufukia zitaandaliwa na mteja atafahamishwa na atapewa namba ya malipo akalipie kisha tayari atakuwa amekamilisha taratibu zote na yupo tayari kwa kuunganishiwa huduma ya majisafi.

TAHADHARI: EPUKA VISHOKA FIKA OFISINI KUPATA HUDUMA HII

Kuna namna nyingi ya kuweza kutufikia ili kutoa taarifa za uvujaji na masuala mengine kama ifuatavyo:

 1. Unaweza kutoa taarifa juu ya kuvuja maji, kuziba kwa mtandao wa majitaka, na wizi wa maji kwa kupiga namba za bure 0800110111
 2. Unaweza kutoa taarifa kwa kufika ofisi za TANGAUWASA zilizokaribu nawe.
 3. Unaweza kutoa taarifa kwa mtumishi yeyote wa TANGAUWASA kuhusu suala au tatizo lolote linalokutatiza