MRADI WA KUBORESHA HALI YA UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI MUHEZA

Imewekwa: Jul, 31 2023

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (TANGA UWASA) inatekeleza mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji huduma ya maji katika Mji wa Muheza wenye gharama ya TZS Milioni 700.

Mradi huo umelenga utekelezaji wa kazi kuu za kukarabati miundombinu na kuendeleza mitandao ya mabomba yenye ukubwa wa inchi 4 hadi 12 katika maeneo ya kata za KWEMKABALA, TANGANYIKA NA MAJENGO ambapo zaidi ya wakazi 24,700 wa maeneo hayo wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo.

TANGA UWASA inatekeleza mradi huu kwa kutumia Force Account ambapo mpaka sasa jumla ya kilomita 7.2 za mabomba zimekwishalazwa na lengo kuu ikiwa ni kulaza mabomba yenye urefu wa Kilomita 7.5 hali itakayo wawezesha wananchi kupata huduma karibu na makazi yao kwa tofauti na sasa ambapo wanapata huduma kwa umbali mrefu.