UTEKELEZAJI MRADI WA MAJI MIJI 28 - PANGANI

Imewekwa: Sep, 26 2023


Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (TANGA UWASA) imeanza rasmi hatua za awali za utekelezaji wa mradi wa Maji wa Miji 28 katika Mji wa Pangani kwa utekelezaji wa kazi za usafishaji wa eneo, uhamishaji wa mabomba na uchimbaji wa msingi kwa lengo la kuandaa eneo litakaotumika katika ujenzi wa tangi kubwa la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 500,000 katika eneo la Boza.

Utekelezaji wa mradi huo unasimamiwa na TANGA UWASA kwa kushirikiana na Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya WAPCOS na Mkandarasi wa Ujenzi kutoka kampuni ya JWIL INFRA Ltd, ambapo kukamilika kwa mradi huu kutawezesha wananchi wa wilaya ya Pangani kupata huduma ya maji ya uhakika na kuondokana na adha ya mgao wa Maji na matumizi ya maji ya chumvi.


MWISHO.