Mabayani Dam - Pande Tanga
Sigi Water

UTARATIBU WA KUUNGANISHWA KATIKA MFUMO WA MAJI TAKA


1.Hatua za kufuata:

 • Mteja atajaza fomu ya maombi ya kuunganishiwa katika mfumo wa maji taka .Fomu zinapatikana katika dirisha la huduma kwa wateja.
 • Wataalam wa mamlaka watafanya ukaguzi (survey) kwenye Eneo (nyumba) ya mteja na kutayarisha gharama.
 • Mteja anaweza kupata taarifa za ukaguzi au gharama za kuunganishiwa katika mfumo baada ya siku nne kuanzia tarehe aliyojaza fomu ya maombi. Taarifa ,gharama au maelekezo yoyote kuhusu huduma mteja aliyoomba yatapatikana dirisha aliloombea huduma.
 • Gharama zote zinazohusika zitalipwa katika Mamlaka na mteja atapewa risiti inayolingana na malipo atakayoyafanya.

TAHADHARI!! Mamlaka haitahusika na mapatano au malipo yoyote yatakayofanywa nje ya utaratibu wa mamlaka.

 

2.Gharama zitakazohusika:-

 1. Gharama za kuunganishwa kwenye mtandao wa maji Taka (connection fees)
 2. Gharama za Vifaa zinazojumuisha bomba za maji Taka na viungio vinavyohitajika kuunga bomba la nyumbani kwenye mtandao wa Majitaka.
 3. Gharama za kuchimba na kufukia mtaro.
 4. Gharama za usimamizi (supervision charge)
 5. Gharama za uwakala (agency fees)

Endapo mteja atafanya malipo atastahili kupata huduma hiyo ndani ya siku nne kuanzia tarehe atakayokuwa amefanya malipo.

 

3. Mambo muhimu ya kuzingatia kwa wateja wenye mabomba ya maji taka:

 • Usiweke taka ngumu ya aina yoyote katika sehemu za kunawia mikono ,bafu au karo la kuoshea vyombo.
 • Hakikisha kuwa sehemu zote zinazopitisha maji taka zina machujio (screen) ili kuzuia takataka zisiingie kwenye chemba au mfereji wa majitaka.
 • Hakikisha kuwa chemba zako za maji taka zina mifuniko ili kuzuia kuingia kwa vitu vinavyoweza kusababisha kuziba kwa mifereji hiyo.
 • Kama maji ya mvua yanaingia katika mfumo wa mfereji wako wa maji taka,hakikisha kuwa umetengeneza chemba ndogo ya kutuliza takataka na uweke chekecheke (chujio)katika tundu la kupeleka maji katika maji katika katika mfereji wa maji taka.
 • Ni marufuku kumwaga mafuta ya aina yoyote kwenye mfereji wa maji taka.
 • Hakikisha kuwa mabomba yako ni salama wakati wote na toa taarifa mara tu unapoona dalili za kuvuja kwa bomba.
 • Ni marufuku na ni hatari kufanya matengenezo yoyote kuhusiana na mfereji wa majitaka bila kibali au maelekezo ya mamlaka.

Ukiwa na maulizo yoyote kuhusu maelezo haya wasiliana na ofisi ya Uhusiano na wateja.