Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TANGA

(Tanga UWASA)

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
/

Uboreshaji wa Miundombinu ya Maji awamu ya III

Imewekwa: 02 November, 2024
Uboreshaji wa Miundombinu ya Maji awamu ya III

Mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji huduma ya maji Tanga Awamu ya Tatu kupitia ufadhili wa Hatifungani ya Kijani (Tanga Water Green Bond) unathamani ya Shilingi Bil. 53.12 na unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya Majisafi na Salama kwa wananchi, kukarabati na kuendeleza Miundumbinu ya Majitaka katika maeneo ya Jiji la Tanga na Utunzaji wa Mazingira katika chanzo cha Mto Zigi kwenye milima ya Amani-Muheza ambapo wananchi zaidi ya 555,313.62 wa Jiji la Tanga, na Miji ya Muheza, Pangani na Mkinga watanufaika na kukamilika kwa mradi huo. 

Kazi zinazotekelezwa katika mradi huo zinahusisha;

1. Kukarabati na kupanua mtambo wa kusukuma Maji Mabayani kutoka uwezo wa sasa wa mita za ujazo 42,000/siku hadi kufikia mita za ujazo 72,000/siku. 

2. Kulaza bomba kubwa lenye kipenyo cha milimita 600 kwa urefu wa kilomita 6.4 kutoka Kituo cha Kusukuma Maji Mabayani hadi kituo cha Kusafisha na Kutibu Maji Mowe.

3. Kukarabati na kupanua Mtambo cha Kusafisha na Kutibu Maji Mowe kutoka uwezo wa sasa wa mita za ujazo 45,000/siku hadi kufikia mita za ujazo 60,000/siku.

4. Ujenzi wa Tangi kubwa la Kuhifadhi Maji lenye uwezo wa mita za ujazo 35,000 katika eneo la Mowe.

5. Kukarabati mtandao wa mabomba uliochakaa katika maeneo mbalimabli ya Jiji la Tanga kwa urefu wa kilomita 110.

6. Kuendeleza kwa mtandao wa mabomba kwa urefu kwa kilomita 60 kwa maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma ya maji katika Jiji la Tanga (30km), Muheza (15) na Pangani (15km).

7. Kufunga mita za malipo kabla (prepaid water meter) 10,000 kwa wateja mablimbali wa Jiji la Tanga, Muheza na Pangani.

8. Kukarabati na kuendeleza mtandao wa Majitaka kwa urefu kilomita 3 katika maeoneo mbalimbali ya Jiji la Tanga.

9. Kutunza mazingira katika vyanzo vya mto zigi kwa kupanda miti zaidi ya 100,000 na kuongeza vijiji vya utunzaji wa mazingira (UWAMAKIZI) kutoka 21 hadi kufikia 31.