WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA - OFA YA KUREJESHA MAJI BILA TOZO
Imewekwa: 07 October, 2026
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja 2026, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafı na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) anawataarifu kuwa kutakuwa na OFA maalumu kwa wateja waliositishiwa huduma ya maji
kutokana na madeni, kurejeshewa huduma bila kulipia tozo ya kurejeshea huduma (Re - connection fee).
Hivyo Mkurugenzi Mtendaji anawasihi wateja waliositishiwa huduma kufika kwenye ofisi za Tanga UWASA zilizo karibu nao, ili kuingia makubaliano ya kulipa madeni yao na kurejeshewa huduma bila tozo.
Ofa hii itaanza tarehe 06 - 16 Oktoba, 2026.

