Mabayani Dam - Pande Tanga
Sigi Water

FAHAMU UKWELI KUHUSU MATUMIZI YA META YA MAJI


Mteja anastahili kulipa bili inayotokana na matumizi yake halisi .Matumizi halisi ya mteja yanapimwa kupitia meta ya  maji ambayo ni mali ya mamlaka,Wateja wote wa maji safi na maji taka jijini Tanga wanalipa kutokana na matumizi yao  halisi yanayopimwa kupitia meter zao. Meta ya maji humsaidia mteja kuweza kufuatilia na kudhibiti matumizi yake ya maji .

1.Masharti ya kufungiwa meta (dira) ya maji:

 •     Kuanzia siku mteja atakapo fungiwa meter, meta hiyo
            itakuwa chini ya dhamana yake na anapaswa kuhakikisha
            Usalama wake.Endapo meta itaharibiwa au kupotea
            mteja atalazimika kulipa gharama ya ununuzi wa meta
            nyingine.
 •     Meta (dira) ya maji itafungwa na mafundi wa Mamlaka tu.
 •    Mteja haruhusiwi kuifungua,kuitengeneza ,kuihamisha
            mahali itakapofungwa au kuruhusu watoto ama mtu
            mwingine yeyota kuichezea.
 • Ni kosa mteja au mtu yeyote ambaye si mtumishi wa
           mamlaka kufanya marekebisho yoyote katika  meta ,na
           yeyote ataepatikana na kosa hilo atakatiwa maji
           ikifuatiwa na hatua nyingine za kisheria.
 •    Mteja atawajibika kusaini mkataba wa maandishi
            wakati wa kufungiwa meta ya maji.Mteja atapatiwa
            nakala ya mkataba huo na atapaswa kuutunza na
            kuutoa wakati wowote utakapohitajika.

2. Mambo ya kufanya endapo meta itaibiwa.

    1).  Mteja atawajibika kutoa taarifa Polisi mara moja na
          kupeleka taariza za wizi huo katika ofisi za
          mamlaka ,kitengo cha (kanda husika).

    2).  Mteja atapaswa kulipa gharama ya kununua dira
         (meta) nyingine ya maji kwa itakayokua inauzwa
         kwa wakati huo. Endapo meta hiyo itapatikana ,
         gharama alizolipa mteja zitarejeshwa kwenye
         akaunti yake ya maji.

 

TAHADHARI!
Ni marufuku mteja kujiungia maji baada ya kuibiwa meta. Endapo mteja atajiungia maji baada ya kuibiwa meta atachukuliwa hatua za kisheria kwa kosa la wizi wa huduma.

NB” Tunza dira ya maji” na jiwekee utaratibu wa kusoma meta (dira) yako ya maji ili uweze kufuatilia matumizi yako ya maji na kupata ankara sahihi inayolingana na maji yaliyotumika.....Jinsi ya kosoma Meter

 

Ukiwa na maulizo yoyote kuhusu maelezo haya wasiliana na ofisi ya Uhusiano na Wateja

Ukiwa na maulizo yoyote kuhusu maelezo haya wasiliana na ofisi ya Uhusiano na wateja.